Jumatatu , 10th Nov , 2014

Halmashauri ya wilaya ya Mwanga nchini Tanzania itayasimamisha makampuni yote ya ujenzi wa barabara yanayofanya kazi zake chini ya kiwango na hayatapewa tenda kuanzia sasa katika wilaya hiyo.

Moja ya Majengo ya barabara zilizopo mkoani Kilimanjaro

Uamuzi huo umepitishwa na kikao cha Baraza la Halmashauri hiyo kutokana na kuwepo kwa baadhi ya barabara za vijijini ambazo ujenzi wake upo chini ya kiwango ingawa baadhi ya makampuni yamelipwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira wa Halmashauri hiyo Bw, Kiure Msuya amesema, hilo ni moja ya maazimio na kuzitaja barabara hizo kuwa ni shighatini/kisangara juu, lembeni/kilomeni na lang'ata/mwanga.

Diwani wa Kata ya Shighatini Bw, Enea Mrutu amesema, mkandarasi aliyejenga barabara ya shighatini/kisangara juu ingawa amelipwa kiasi cha fedha na kutakiwa airudie upya ujenzi wa barabara hiyo lakini amekataa.