Jumatatu , 9th Nov , 2015

Wakazi wa vijiji 17 vinavyovyozunguka hifadhi ya msitu wa asili (NILO) wameanza kunufaika kwa kupewa miradi mbalimbali ya kilimo cha biashara, ufugaji nyuki na mifugo ili waweze kuhifadhi misitu na kuachana na hujuma za uvunaji kinyume cha sheria

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya (NILO), Bw,Phabian Mkome

Akizungumza katika hifadhi hiyo kuhusu mhifadhi wa hifadhi ya (NILO) Bw. Simon Matula amesema kabla ya kuwapatia miradi hiyo inayofadhiliwa na mfuko wa hifadhi ya milima ya Tao la mashariki,wametoa elimu ili waweze kuzalisha bidhaa zao kwa tija.

Akifafanua kuhusu vikundi vilivyoanza kunufaika Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya hiyo Bw. Phabian Mkome amesema kikundi cha ufugaji nyuki kimeongeza uzalishaji wa asali na hivi sasa sehemu kubwa ya wakazi waliojiunga na vikundi hivyo wameachana na kazi ya uharifu wa mazingira uliokuwa ukifanywa kinyume cha sheria.

Kufuatia hatua hiyo viongoiz wa kikundi cha jitegemee kinachojihusisha na ufugaji nyuki katika kata ya kizara wamesema mradi wa ufugaji wa nyuki umewapa mafanikio kwa kuweza kujipatia kipato kinachowawezesha kuwapeleka shule watoto wao.