Jumatano , 25th Jun , 2025

Shirika la kusaidia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR limesema mataifa yatahitaji kufungua milango yao kupokea idadi kubwa ya wakimbizi mwaka 2026

Umoja wa Mataifa umesema wakimbizi wanaokadiriwa kufikia milioni 2.5 duniani kote watahitaji kutafutiwa makaazi mwaka ujao, katika wakati ambapo Marekani na mataifa mengine yanapunguza wahamiaji.

UNHCR imesema idadi ya wanaohitaji kupatiwa makaazi imepunguwa kiasi mwaka huu kutokana na mabadiliko ya kisiasa yaliyoshuhudiwa  nchini Syria ambako raia wake wameruhusiwa kurejea kwa khiyari nchini humo.

Msemaji wa UNHCR, Shabia Mantoo amesema kuna idadi kubwa ya wakimbizi ambao huenda wakahitaji  kutafutiwa nchi za kwenda  kuishi mwaka 2026, kutoka Afghanistan,Syria,Sudan Kusini, Warohigya kutoka Myanmar na Wakongomani.