
Watanzania wa madhehebu ya Kikristo leo wameungana na waumini wa Kikristo kote duniani kuadhimisha ibaada ya Ijumaa Kuu kukumbuka mateso ya Kristo Yesu miaka takribani 2000 iliyopita.
Baadhi ya Makanisa yaliadhimisha ibaada ya Ijumaa kuu mapema leo asubuhi wakati makanisa mengine yaliendesha ibaada zao kuanzia saa tisa alasiri.
Katika Kanisa la Parokia Mt.Maximilian Maria Kolbe Mwenge Jimbo kuu la Dar es salaam liliendesha ibaada yake saa tisa mchana ambapo Mhashamu Askofu Eusebius Nzingilwa Askofu Msaidizi Jimbo kuu la Dar es salaam aliendesha ibada hiyo ambapo amesisitiza vyombo vya haki kutenda haki bila kufuata mashinikizo na kuwaasa waumini kuwa moyo wa msamaha na kutolipiza ubaya kwa ubaya kwa kuwa Yesu Hakufanya hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa East Africa Television Limited anawatakia Watanzania wote Heri ya Siku Kuu ya Pasaka