
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
Miongoni mwa Wakuu wa Mikoa ambao wameondolewa kwenye nafasi walizokuwepo ni pamoja na Ally Hapi aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Mara, Brigedea Jenerali Marco Gaguti aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mtwara, David Kafulila alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Benelith Mahenge aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Singida, Stephen Kagaigai aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Robert Gabriel aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Meja Jenerali Charles Mbuge aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera na wengine.
Wakuu wapya wa mikoa ni pamoja na Dkt. Raphael Masunga aliyeteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Mara, Nurdin Babu ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro,Halima Omari Dendego Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Albert Chalamila aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera pamoja na wengine.
Miongoni mwa Wakuu wa Mikoa walihamishwa Mikoa ni pamoja na Antony Mtaka aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Queen Sendiga aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Iringa, ambaye sasa amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, pamoja na Martine Shigella aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambaye sasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Katika uteuzi huo wa leo, baadhi wa Wakuu wa Mikoa wamesalia katika Mikoa waliokuwepo awali, ikiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera na Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella.
Mbali na uteuzi wa wakuu wa Mkoa pia Rais Samia amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Mikoa wapya 7, huku makatibu Twala wa Miko 10 wakihamishwa vituo na wengine 9 wakisalia kwenye vituo vyao vya awali.