Jumatatu , 13th Feb , 2023

Wiki moja baada ya tetemeko kubwa la ardhi kukumba Uturuki na Syria, idadi ya watu waliothibitishwa kufariki imeongezeka hadi zaidi ya 37,000

 

 

  Lakini shirika la misaada la Umoja wa Mataifa limeonya kuwa idadi ya mwisho ya vifo kutokana na tetemeko hilo huenda ikaongezeka maradufu ya idadi hiyo.

   Serikali ya Marekani imetoa wito kwa Syria na pande zote zinazohusika kutoa fursa ya kibinadamu mara moja kwa wale wote wenye uhitaji kote nchini humo.

Wakati huo huo, maafisa nchini Uturuki wanasema waranti 113 za kukamatwa zimetolewa kuhusiana na ujenzi wa majengo yaliyoanguka katika tetemeko la Jumatatu

Mpaka mchana wa leo Maafisa kutoka mamlaka ya usimamizi wa majanga nchini Uturuki wanasema watu 31,643 wamekufa huko, wakati kaskazini magharibi mwa Syria idadi hiyo kwa sasa ni 4,300 kulingana na maafisa wa Umoja wa Mataifa.

Idadi hiyo inaendelea kuongezeka kadri tunavyokuripotia taarifa hizi