
Daraja la mto Mwandoya
Akizungumza na wananchi baada ya kukagua ujenzi wa daraja hilo unaotekelezwa na kampuni ya mzawa wa Tanzania ANDIC LTD, Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina, amesema mbali na daraja hilo kunusuru maisha ya watu, lakini pia ni kiungo muhimu katika kukuza uchumi wa wanananchi.
"Namshukuru sana Rais Samia kwa kuridhia hilo (utoaji fedha za dharura kujenga daraja Mto Mwandoya) ndiyo maana tukaletewa hili daraja na kulijenga na kulimaliza, daraja la milioni 304, na leo tunaambiwa ndani ya mwezi mmoja maana yake mvua zinaanza sisi tuna daraja la kupita juu," amesema Mbunge Luhaga