Jumapili , 16th Feb , 2020

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, ameliagiza Jeshi la Polisi mkoani humo kuhakikisha linawachukulia hatua stahiki wale wote walioshiriki katika zoezi la usambazaji wa video mitandaoni, zinazoonesha ubovu wa miundombinu katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

RC Gambo amesema kuwa haikuwa vibaya kukosoa ubovu wa miundombinu hiyo bali haikuwa jambo jema kusambazaa video hizo mitandaoni ili hali kuna viongozi ambao walipaswa kupelekewa taarifa hizo na suala hilo likapatiwa ufumbuzi.

"Changamoto hii ya barabara iko maeneo yote duniani sio Tanzania pekee, wapo baadhi ya watu kama Tour Guide ambao wamekuwa wakitoa taarifa bila kibali cha mamlaka husika, Mataifa mengine siyo kwamba hakuna mabaya, sema wanachagua ni kipi cha kupeleka Duniani, namuagiza RPC awachukulie hatua wale wote wanaochafua picha ya nchi, mimi nawachukulia kama wahujumu uchumi" amesema RC Gambo.

Hivi karibuni zilisambaa video mbalimbali katika mitandao ya kijamii, zikionesha ubovu wa miundombinu ya barabara katika hifadhi hiyo.

Tazama Video hii hapa chini