
Taarifa za kulipwa fidia wananchi waliopisha mradi wa Liganga na Mchuchuma zilitolewa rasmi mapema mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasani kuwasili Mkoani Njombe ambapo Kituo hiki mara maada ya kuwasili wilayani Ludewa kwa Wananchi waliopisha mradi
Akizungumza mwakilishi wa shirika la taifa la maendeleo NDC Bw. Maundi amesema mapema mwezi huu serikali ipo tayari kuanza taratibu za kuanza kuwalipa wananchi walio pisha mradi huo huku Mbunge wa Jimbo la Ludewa Joseph Jamonga akiwataka wananchi kutoa ushirikiano wakati wa uhakiki wa wananchi walio pisha maeneo ya mradi huo kwa muda mrefu