Jumatatu , 22nd Aug , 2022

Waziri Mkuu wa Somalia Hamsa Abdi Barre amesema  atawawajibisha maafisa wa usalama walioshindwa kuzuia shambulizi la mauaji lililotelekezwa na vikosi vya  al-Shabab kwenye hoteli ya  Hayat Hotel huko mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu

Barre  ametoa maelezo hayo kwenye televisheni ya taifa la nchi hiyo baada ya vikosi vya usalama kumaliza mapambano dhidi ya vikosi vya al-Shabab ambayo yalidumu kwa saa 35 kwenye hoteli hiyo maarufu 

Waziri huyo mkuu ameongeza kwamba tukio hilo halikubaliki na kwamba kila afisa usalama ambaye hakutimiza majukumu yake ni lazima awajibike

 
Waziri wa afya nchini humo  Ali Hajji Aden amesema kuwa takribani watu 21 wameuawa kwenye mapambani hayo huku wengine  117 wakijeruhiwa

Waziri mkuu huyo  alifanya ziara ya kuwatembelea waliohjeruhiwa na kwamba walio kwenye hali mbaya zaidi watapelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi

Shambuzli i hilo lililofanywa  wiki iliyopita huku lilitibitishwa na tovuti al shabab, limepelekea wananchi kuikosoa serikali kwa kushindwa kumaliza mara moja mapambano hayo yaliyogharimu maisha ya watu