
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Awadhi Juma,
Kamanda wa Polisi mkoani Kagera Awadhi Juma, amesema kuwa bibi huyo aliuawa Oktoba 15, 2021, na kwamba baada ya watuhumiwa hao ambao ni Robert Berenado (19) na mke wake Benadetha Robert (19) kumuua, walikimbia na kwenda kujificha katika Kijiji cha Kiruruma kilichoko wilayani Karagwe, na baada ya upelelezi kufanyika walikamatwa na polisi Oktoba 31 mwaka huu.
Aidha, Kamanda huyo amesema kuwa jeshi hilo linawashikilia Tawabu Ismail (35) na Joseph Laurian (42), wakazi wa Minziro wilayani Missenyi mkoani humo baada ya kukamatwa wakiwa na mfupa wa mguu na meno ya Tembo kinyume cha sheria.