
Kibao cha Serikali ya Wanafunzi DARUSO
Hatua hiyo ya DARUSO imekuja baada ya Bodi ya Mikopo kutoa taarifa kuwa imekaa kikao cha pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, pamoja na uongozi wa Serikali ya wanafunzi na kukubaliana wanafunzi wawasilishe changamoto zao kwenye vyuo.
Uongozi wa DARUSO kupitia ukurasa wao wa Twitter umeandika kuwa "kwakuwa katika kikao hicho viongozi wa DARUSO hawakuwa na agenda tofauti na madai ya awali na kwakuwa HESLB katika ufafanuzi wake imeonesha kupuuza baadhi ya hoja pamoja na kutulisha maneno, tunawataarifu kwamba msimao wetu ni uleule na yamebaki masaa 48"
Awali katika taarifa waliyoitoa Bodi ya Mikopo wamesema kuwa "Mlipaswa kutoa taarifa kwa mamlaka husika ikiwemo Menejiment ya Chuo chenu, au mngetufuata sisi tungeyafanyia kazi na si kutupatia maelekezo ndani ya saa 72."
#HABARI Uongozi wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (DARUSO), umesema haujaridhika na ufafanuzi uliotolewa na Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu Nchini (HESLB), na kueleza bado wanaendelea na msimamo wao uleule na sasa yamebaki masaa 48.
— East Africa Radio (@earadiofm) December 17, 2019