Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Bwiru
Moto huo unaodaiwa kuzuka majira ya saa 3:36 usiku ambapo kwa kawaida muda huo wanafunzi wote walikuwa madarasani wanajisomea ghafla wakasikia kengele ya dharura ndipo wakatoka nje na kuona bweni hilo ambalo walikuwa wanalala wanafunzi wa kidato cha kwanza likiteketea kwa moto.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel, amefika katika shule hiyo na kusema uongozi wa mkoa utahakikisha unasimamia taratibu zote na kuhakikisha wanafunzi hao wanapata sehemu ya kulala ikiwemo na vifaa vyao vilivyoteketea kwa moto ili kuhakikisha wanaendelea na masomo yao.