Jumatano , 14th Oct , 2020

Katika kuadhimisha miaka 21 ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Jijini Dar es Salaam imefanya mafunzo maalum kwa wanafunzi zaidi ya mia sita ili kujifunza falsafa za Baba wa Taifa ikiwemo misingi ya haki na amani.

Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake.

Akizungumzia dhumuni la mafunzo hayo, Anastasius Liwew, ambaye ni Mkuu wa Maonyesho Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni  amesema kuwa lengo ni kuwaandaa wanafunzi hao kuwa Wazalendo, wenye upendo na wakue katika misingi ya Haki na Amani.

Mwalimu Hamis Matalla ambaye ni mmoja ya walimu walioleta wanafunzi katika mafunzo hayo, amesema kuwa watoto wakiandaliwa mapema na kupewa fursa ya kujifunza falsafa za Baba wa Taifa tutaongeza kizazi chenye amani na upendo.

Wanafunzi waliopatiwa mafunzo hayo wamumuelezea Baba wa taifa kama kiongozi aliyepigania Uhuru na umoja na kupinga vitendo vya unyanyasaji.