
Jeshi hilo limeongeza kuwa wanajeshi wengine 50 walijeruhiwa wakati wa makabiliano hayo na wanaendelea kutibiwa.Aidha, limesema miili 18 ya magaidi ilikusanywa katika kambi hiyo baada ya shambulizi.
Eneo la Djibo lina wakaazi 30,000, lakini kwa miezi mitatu limekuwa limetengwa, huku wanamgambo wakidhibiti barabara kuu baada ya kulipua madaraja.Shambulizi dhidi ya msafara wa misaada uliokuwa ukielekea eneo hilo mnamo Septemba 26, lilisababisha vifo vya watu 37, miongoni mwao wakiwa wanajeshi 27.
Tangu tukio hilo, madereva 70 wa malori ya kusafirisha misaada bado hawajulikani waliko.