Jumatatu , 1st Aug , 2016

Rais wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli, ametoa wiki tatu kwa Wizara husika kuhakikisha wanatoa mabaki ya mawe ya dhahabu maarufu kama Magwangala na kuyagawa kwa wananchi wa Mkoa wa Geita.

Rais wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli.

Agizo hilo amelitoa Mkoani Geita, katika uwanja wa kalangala wakati akihutubia wananchi na kuwataka viongozi mkoani humo kupanga mikakati ya kuhakikisha mabaki hayo yangawiwa kwa wananchi ili nao wafaidike na rasimali za taifa.

Rais Magufuli ametoa Onyo kwa viongozi watakaohusika na ugawaji wa Magangwala kwa wananchi na kusema anatakae onekana ni kikwazo basi hatositia kumuondoa mara moja.

Katika hatua nyingi rais Magufuli amegusia kudorora kwa zao la Pamba ambapo ameitaka bodi ya Pamba kuhama Dar es Salaam, na kwenda katika mikoa inayolima pamba ili kufufua zao hilo liweze kuwa chachu ya kuinua uchumi wa nchini.