
Picha za SaTelite kutoka TMA zikikionesha Kimbunga JOBO
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa TMA, Dkt. Agnes Kijazi, amesema kuwa hadi kufikia tarehe 25/04/2021 kimbunga hicho kitakuwa kimetua maeneo ya Dar es Salaam na mara kinapotua hupunguza nguvu sana.
"Kwa sasa hivi ile nguvu ya upepo ni kilomita 90 kwa saa, tunataraji kesho itakuwa 70km kwa saa na wakati kinatua Dar es Salaam endapo mifumo ya hali ya hewa itakuwa haina mabadiliko nguvu itakuwa 60km kwa saa, ambao ni upepo mkubwa unaoweza ukaleta athari," amesema Dkt. Agnes Kijazi.
Dkt. Agnes ameongeza kuwa, “Upepo wa kilomita 60 kwa saa ni upepo ambao kwa boti ambazo zipo baharini ni wakachukua tahadhari lakini pia hata majengo kama mtu anaona kwamba jengo lake haliwezi kustahamili ni vizuri kuwa katika maeneo ambayo ni salama".
Awali akielezea kuhusu jina la kimbunga la Jobo amesema wana utaratibu wa kuvipa majina vimbunga na huo ni utaratibu wa kidunia huku akiwasisitizia wanachi kuchukua tahadhari zinazotolewa na mamlaka hiyo juu ya hali inayoendelea.