Ijumaa , 18th Feb , 2022

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema kwamba kwa wale wakazi wa wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, wanaotaka kuhama kwa hiari yao wajitokeze na waseme wanataka kwenda wapi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na viongozi na wananchi wa tarafa ya Ngorongoro kwenye kikao cha ndani kilichofanyika makao makuu ya zamani ya NCAA, wilayani Ngorongoro.

"Suala la idadi ya watu ni kubwa, kumbe huko nyuma kulishakuwa na mapendekezo yeyote anayeona anaweza kuishi mahali pengine yuko huru kusema, kama yuko mtu wa aina hiyo, awe huru kwenda kwa Mkuu wa Wilaya kajiandikishe na serikali itamhudumia vizuri, hayo ni maamuzi ya mtu binafsi, kusiwe na mtu wa kumshinikiza fulani asifanye maamuzi yake, kama yupo aachwe afanye maamuzi yake, aseme anataka kwenda wapi na sisi tutamhudumia," amesema Waziri Mkuu.