
Mkurugenzi wa habari kutoka Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi nchini Tanzania (TACAIDS) Bw. Jumanne Isango (kulia) akimkabidhi cheti cha ushindi wa uandishi wa habari bora za Ukimwi, mwandishi Erbenezer Mende.
Hayo yameelezwa jijini Dar-es-Salaam na Mkurugenzi wa Urakibishi na habari kutoka Tume ya kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) Bw. Jumanne Isango wakati tume hiyo ilipokutana na viongozi mbalimbali wa kisiasa kwa lengo la kuwapa mafunzo mbalimbali na kuwaeleza hali halisi ya ugonjwa wa Ukimwi hapa nchini.
Takwimu za ugonjwa wa ukimwi kwa mwaka 2011 – 2012 zinaonyesha kwamba mkoa wa Njombe unaogoza kwa kuwa na asilimia 14.8 ukifuatiwa na mkoa wa Iringa asilimia 9, Mbeya asilimia 9, Shinyanga asilimia 7.4 Ruvuma asilimia 7 na jiji la Dar es salaam ni asilimia 6.9.