Jumatatu , 16th Sep , 2019

Mwenyekiti Kijiji cha Mlingotini, maarufu kama Kijiji cha 'Wachawi' Hassan Pembe, amesema Kijiji chake kimekuwa kikitembelewa na watu mbalimbali, kwa nia ya kupata huduma za kienyeji.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo miongoni mwa makundi yanayoongoza kwenda kupata huduma hiyo, ni kundi la wanawake na viongozi wa kisiasa, ambao wengi wao wanafika ili kupewa tiba.

Akizungumza katika Kipindi cha East Africa Breakfast cha EA Radio, Mwenyekiti Hassani Pembe, amesema kuwa "Kiuhalisia wanawake ndiyo wengi wanaongoza kuja hapa kwa ajili ya kupata huduma za kienyeji."

"Kuna watu maarufu wanaokuja hapa kupata huduma, utakuta Waziri na viongozi wa kisiasa wamekuja hapa jambo lake limefanikiwa basi yeye anatupa shukrani ya kutujengea barabara au kutuletea umeme." amesema Mwenyekiti Pembe.

Fuatilie mahojiano kamili hapo chini