Jumanne , 13th Oct , 2015

Pamoja na ongezeka kubwa la wanawake kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu bado kuna changamoto na vikwazo vingi vinavyomkabili hasa mgombea mwanamke,ambavyo tayari vimeshawasilishwa kwenye tume ya uchaguzi(NEC) kwa ajili ya utatuzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha sheria na Haki za Binadamu(LHRC) Dr Helen Kijo Bisimba.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na wakili wa dawati la jinsia na watoto kutoka kituo cha sheria na haki za binadamu nchini (LHRC)Bi. Naemy Silayo kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo wanawake wagombea katika mchakatowa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika 25 mwezi na kuongeza kuwa tayari wameanza kushughulikia changamoto mbalimbali wananzokutana nazo wagombea wanawake.

Aidha Bi Naemy ameongeza kuwa kwa upande mwingine katika tafiti zao mbalimbali wanazofanya juu mchakato unaoendelea kuelekea uchaguzi mkuu wamebaini mapungufu mengine ya ukosefu wa rasilimali pesa katika kujitangaza zaidi na kuvitaka vyama viwape kipaumbele wanawake wenye nia ya kugombea.

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo Bi. Godliver Manumbu amesema kuwa changamoto kubwa inayomkabili mwanamke ni uhitaji wa rasimali ambazo wanawake wengi hawana na hizi zinapelekea uchaguzi huu usiwe huru na wa haki kwa mwanamke.