Jumatano , 15th Jun , 2016

Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi,NEEC limeanzisha mkakati maalumu wa utoaji wa mikopo kwa wanawake kupitia taasisi ya fedha kupitia vikundi vya Vicoba na Saccos.

Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi,NEEC limeanzisha mkakati maalumu wa utoaji wa mikopo kwa wanawake kupitia taasisi ya fedha kupitia vikundi vya Vicoba na Saccos.

Katibu mtendaji wa baraza hilo Beng’i Issa alisema jijini Dar es salaam kuwa kuwa mpango huo unafanyika kwa baraza kuweka dhamana ya fedha za serikali kwenye taasisi za fedha na wakopaji kupatiwa mikopo yao kwa riba nafuu ya asilimia 11.

Bw Issa amewataka wanawake kutumia fursa hiyo ili kuongeza mitaji yao na kuwa wanawake hao wataongezewa uelewa katika masuala ya mnyororo wa thamani kwenye mazao, masoko ya kimataifa, fursa na kuimarisha biashara.

Ameongeza kuwa hadi kufikia sasa watanzania takribani milioni 11. 1 wamenufaika na fursa hizo katika ngazi ya kaya, kutokana na wanajamii kujiunga na vikundi hivyo.