Alhamisi , 4th Feb , 2016

Wanazuoni na Wachambuzi wa masuala ya siasa wameonyesha hali ya wasiwasi wa hali ya kisiasa visiwani Zanzibar baada ya Tume ya Uchaguzi visiwani humo kutaka uchaguzi urudiwe na kusema kuwa hali hiyo inaweza kusababisha mgogoro mkubwa visiwani humo.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba

Akiongea jana Jijini Dar es Salaam Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba amesema kuwa ili kutuliza mzozo huo wa kisiasa visiwani humo ni bora akapatikana msuluhishi watatu ambaye anaweza kusuluhisha mgogoro huo ili kuepuka damu kumwagika.

Jaji Warioba amesema kuingia katika kutafuta uongozi mpya bila kuwa na maridhiano ya vyama vyote Zanzibar inaweza ikarudia machafuko kama yaliyotokea katika kipindi cha miaka ya nyuma jambo ambali litaichafua Tanzania.

Aidha waziri mkuu huyo mstaafu amesema kuwa vyama vinapaswa kuachana na dhana ya kwamba malumbano hayo ni ya kivyama zaidi na badala yake watoke katika dhana hiyo na waweze kuwajali wananchi wa visiwa hivyo na kujua ni kitatokea baada ya Uchaguzi.

Kwa upande wake Prof. Mwesiga Baregu amesema licha ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC kutoa sababu tisa za kufuta uchaguzi huo lakini alikiuka katiba ya Zanzibar pamoja na sheria za uchaguzi halali ambayo inaweza kuchafua siasa za Tanzania.