Jumapili , 18th Dec , 2016

Wakuu wa Wilaya (Ma-DC) na Wakurugenzi nchini, ambao hawajakamilisha kutengeneza madawati, yanayokidhi idadi ya wanafunzi katika shule za maeneo yao, wamepewa siku 14 kukamilisha kazi hiyo.

Wakuu wa wilaya na wakurugenzi, watakaoshindwa kutimiza agizo hilo hadi ifikapo Desemba 30, mwaka huu, watakuwa wamejifukuzisha kazi wenyewe.

Agizo hilo lilitolewa jana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Arumeru katika ziara yake ya kikazi mkoani Arusha.

“Wale ambao watashindwa kufanya hivyo, watakuwa wamejifukuzisha kazi wenyewe” alisema Waziri Mkuu.