Jumatano , 5th Oct , 2022

Baadhi ya wachambuzi wa siasa,wasomi na wachumi wamesema kutokana na unyeti wa Wizara ya tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI wameshauri Wizara hiyo ingetenganishwa ama wameshauri ngazi za mkoa na wilaya wapewe maamuzi ya Moja Kwa Moja kuliko kusubiria serikali kuu..

Angela Kairuki-Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za mitaa

Hatua hii imefikiwa baada ya ripoti kuonesha  Mara Kwa mara ubadhilifu ukifanywa katika Halimashuri mbalimbali huku nyingi zikishindwa kukusanya mapato tarajiwa.

Watalaamu hawa wanasema huenda ikawa ni sababu ya kubadilishwa Sana Kwa mawaziri kwenye Wizara hiyo Kwa tafsiri ya kushindwa kufikia matarajio kwenye ukusanyaji wa mapato.

"kuna tatizo mahala maana kule chini wakifanya matatizo wanaacha mzigo mzima kuwa wa wizara na serikali kuu sasa ushauri wanga nadhani wangeaacha maamuzi ya moja kwa moja ngazi za wilaya na mkoa ili kupunguza mzigo huu"alisema Dkt Respicius Shumbusho-Mhadhiri Idara ya Sayansi ya siasa na utawala wa Umma.

Itakumbukwa Kwa mwaka 2021-22 bajeti ya TAMISEMI ilifikia Hadi Shilingi trilioni saba ikitajwa kuwa bajeti kubwa sana kulingana na  Halimashuri zingine kushindwa kukusanya makusanyo licha ya matumizi ilizonazo

Kwa takribani ndani ya Miezi 19 Wizara ya TAMISEMI wamebadilishwa mawaziri wanne akiwemo Dkt Selemani Jaffo,Ummy Mwalimu, Innocent Bashungwa na sasa Mhe  Angela Kairuki..maswali ni je atafikia matarajio hususani hasa katika ukusanyaji wa mapato na udhibiti ubadhilifu ambao tumekuwa tukiusikia katika ripoti za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali?