Alhamisi , 1st Dec , 2022

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limefuta matokeo yote ya watahiniwa 2194 sawa na asilimia 0.16 ya watahiniwa milioni 1.35 waliofanya mitihani, baada ya kubainika wamefanya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2022.

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) Ramadhani Amasi.

Hayo yamebainishwa hii leo Desemba Mosi, 2022, jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Ramadhani Amasi.

"Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limefuta matokeo yote ya watahiniwa 2194 sawa na asilimia 0.16 ya watahiniwa milioni 1.35 waliofanya mitihani, ambao wamebainika kufanya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2022" amesema Kaimu Katibu Mtendaji

Aidha Baraza hilo pia limevifungia vituo 24 vilivyothibitika kufanya udanganyifu, "Baraza la mitihani limevifungia vituo vya mitihani 24 ambavyo vimethibitika kupanga na kufanya undanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2022 na vimefungiwa hadi hapo Baraza litakapojiridhisha ni salama kwa uendeshaji wa mitihani ya kitaifa,".