Jumatano , 27th Jan , 2016

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibari imesema itawafungia na kuwapokonya leseni wafanyabiashara watakaobainika kubagua wananchi kwa kisingizio cha kisiasa.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa rais Mhe. Mohammed Abood Mohammed.

Kauli imekuja kufuatia taarifa kuzagaa ya kwamba tokea kutolewa tamko la kuridiwa uchaguzi kuna baadhi ya wafabiashara visiwani hawauzi baadhi ya watu wanapokwenda kwenye maduka hayo.

Tamko hilo limetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa pili wa rais Mhe. Mohammed Abood Mohammed alipokua akizungumza na viongozi wa kiserikali wa mkoa wa kusini Pemba.

Aidha Mhe Abood amesema kuwa serikali imejipanga kuweka ulizni wa kutosha ili kuhakikisha amani na utulivu inadumu wakati wote wa Uchaguzi ,kuhesabu kura na hata baada ya Uchaguzi.

Hapo awali viongozi hao wa serikali wakiwemo mashekha pamoja na wazee wa CCM kumuomba waziri huyo kuweka ulizni wa kutosha wakati wa uchaguzi hasa katika maeneo ya vijijini.