Jumamosi , 31st Aug , 2019

Jeshi la Polisi nchini limewatahadharisha wale wote watakaoleta vurugu wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa watachukuliwa hatua mara moja.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini David Misime, ambaye amesema kuwa watu wakifuata sheria chaguzi zote nchini zitabaki kuwa na amani.

“Wale ambao wanahisi watatingisha kiberiti kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa, sisi tumejipanga vizuri kukabiliana nao kwa nguvu zote kwa jinsi ambayo tutazidi kupokea nguvu toka kwao” amesema Misime.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo alitangaza na kusema kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika Novemba 24, 2019.