Jumamosi , 27th Aug , 2022

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dk.Selemani Jafo amegiza kuanzishwa kwa oparesheni kabambe yakuteketeza mifuko ya plastick katika maeneo mbalimbali nchini

Dk.Selemani Jafo ameagiza wale wote ambao wamekuwa wakitumia vifungashio kama vibebeo kuacha kufanya hivyo mara moja huku akizitaka kamati za ulinzi za mikoa na wilaya kuchukua hatua kwa watakao kiuka

Waziri Jafo ametoa agizo hilo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na wajumbe wa baraza la mazingira (NEMC) kuhusu utekelezaji wa sheria ya mazingira ambapo amesema kampeni hiyo itatekelezwa katika maeneo ya maduka, sokoni, magulio, mabucha na mabucha ya nyama na samaki.

Aidha ameagiza wakuu wa mikoa kupitia kamati za ulinzi na usalama kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa pamoja na kudhibiti uingizwaji wa vibebeo hivyo mipakani sambamba na kuwashirikisha viongozi wa masoko kama anavyoeleza

Akizungumza na EATV  meneja kanda ya ziwa Victoria Jerome kayombo amesema changamoto kubwa ya matumizi ya mifuko ya plastiki ni wazalishaji na wasambazaji ambao wamepeleka vifungashio kwenye masoko na kugeuza kuwa vibebeo na hivyo kufanya matumizi ambayo hayakukusudiwa.

Agizo hilo linakuja kufuatia matumizi holela ya vifungashio jambo ambalo limesababisha uchafuzi wa mazingira na kwenda kinyume na utekelezaji wa sheria ya mazingira nchini