Jumamosi , 8th Feb , 2020

Watu watano wafariki Dunia kufuatia Mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Serengeti mkoani Mara huku Kaya 400 zipo hatarini kukumbwa na njaa kufuatia mazao mashambani kusombwa na maji.

Mafuriko (Picha si halisi)

Wakizungumza kwa masikitiko wanakijiji wa Vijiji 5 vya Kata ya Kisaka wamesema kuwa mvua za mwaka huu zimeathiri vikali mazao yao, kwani yalikuwa yamefikia hatua ya uvunaji.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurudin Babu amewataka wananchi kuchukua tahadhari hasa katika kipindi hiki cha msimu wa mvua.