Alhamisi , 30th Jul , 2015

Watu watatu wamelazwa katika hospitali teule ya shirati wilayani rorya baada ya kujeruhiwa vibaya katika ugomvi ambao unadaiwa kuhusishwa na kampeni za kisiasa za wagombea wa ubunge wa Chama Cha Mapindizi katika jimbo la Rorya

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya alieshika mic Samwel Kiboye maarufu kama Namba 3akizungumza na wananchi wa Kata ya Utegi wilayani humo.

Mmoja ya majeruhi wa tukio hilo,amesema walishambuliwa na chupa huku wakitishiwa kukatwa mapanga muda mfupi baada ya kumalizika mkutano wa kampeni za CCM, katika eneo hilo.

Hata hivyo mwenyekiti wa CCM, wilaya ya Rorya Bw. Samwel Kiboye, amekiri kupata taarifa hizo kuhusu wafuasi wa mmoja ya wagombea kununuliwa silaha za jadi kwa ajili ya kushawambulia vijana wa wagombea wengine na kusema mbali na tukio hilo kufikishwa katika vyombo vya dola pia chama hicho kitachukua hatua kali kwa wahusika

Aidha baada ya Tukio hilo mmoja wagombea Lameck Airo akitishia kujitoa kugombea ubunge endapo vitendo hivyo havitadhibitiwa .