Ijumaa , 24th Feb , 2023

Watoto wanne wamepotea kwa kuzama katika mto Ruiche na wengine wawili kuokolewa baada ya mtumbwi uliokuwa umewabeba kupinduka na kuzama katika mto huo uliopo Kata ya Kagera Manispaa ya kigoma Ujiji.

Mto Ruiche

Watoto hao walikuwa wakielekea shule ya msingi Kagera, ambapo hulazimka kuvuka ng'ambo ya pili kwa kutumia Mtumbwi ambapo nahodha alizidiwa nguvu kutokana na mto huo kujaa maji.

Nahodha wa mtumbwi huo Ndemeye Andrea amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 2:00 asubuhi leo Februari 24, 2023, wakati akiwavusha watoto hao kwenda shule ng'ambo ya pili.

Aidha vikosi vya uokozi kutoka Jeshi la Zimamoto vikiongozwa na mkuu wa wilaya ya Kigoma vinaendelea na juhudi za kuwatafuta, licha ya Kaimu Kamanda wa Jeshi hilo mkoa wa Kigoma kueleza, kuwakosa hadi sasa.