Jumatatu , 27th Feb , 2023

Watu 10 wamenusurika kifo Mtaa wa bank kuu Jijini Mbeya  baada ya nyumba wanayoishi kuteketea kwa moto majira ya saa tisa usiku  kwa kile kinachodaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme

Wakielezea tukio hilo manusura na mashuhuda wa ajari  hiyo wamesema majira ya saa tisa usiku wa kuamkia leo  wakati mvua ikiendelea kunyesha ghafla ilipiga radi na umeme ukakatika na baada ya kurejea walianza kusikia harufu ya vitu vikiungua 

Akizungumza kwa niaba ya kamanda wa jeshi la zima moto na ukoaji    Ramadhan Sebombo  amesema walifanikiwa kuzima moto huo ingawa baadhi ya vyumba na mali zake zimeungua huku akisisitiza wananchi kutoa taarifa haraka yanapotoea matukio kama hayo ili kunusuru mali zao