
Wapiganaji waliosheheni zana za kijeshi walilivamia eneo la kijeshi la Frontier Corps huko Muslim Bagh, jimboni Balochistan na kuteka familia tatu.
Hadi wakati huu hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, lakini makundi ya yanayopigania kujitenga kwa jimbo hilo la kusini magharibi wamekuwa mara kwa mara wakivilenga vikosi vya usalama.
Pakistan imeshuhudia ongezeko kubwa la mashambulizi tangu kundi la Taliban la Afghanistan kurejea madarakani mwaka 2021.