Jumapili , 23rd Jan , 2022

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma, Onesmo M. Lyanga amethibitisha kutokea kwa tukio la kuuawa kwa watu watano wa familia moja na watu wasiojulikana katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma, Onesmo M. Lyanga

Kamanda Lyanga amesema kuwa tukio hilo liligundulika jana na kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo.