
Picha ya ajali ya basi la abiria lililogongana na fuso eneo la Ibadakuli Shinyanga
Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga Leonard Nyandahu amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva la basi kutofuata sheria za barabarani na kuendesha kwa mwendo kasi na kusababisha ajali hiyo eneo la Ibadakuli Shinyanga.
Aidha Kamanda Nyandahu amesema ajali hiyo imehusisha basi la Kampuni ya Super Najmunisa yenye namba za usajili T.413 DAY likitokea Dar es salaam kuelekea Jijini Mwanza, na Fuso yenye namba za usajili T.123 DJH likitokea Mwanza kwenda Dar es salaam likiwa limebeba mzigo wa dagaa.