Jumamosi , 7th Jan , 2023

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuwa mwaka huu serikali haitakuwa na msamaha kwa mtumishi yoyote ambaye atakwenda kinyume na miongozo na ambaye hatozingatia maadili na weledi katika utumishi wake

Waziri Ummy amesema serikali imeanza kuona ongezeko la uzembe na kutozingatiwa kwa maadili kwa baadhi ya watumishi wa afya nchini

Kauli ya Waziri Ummy imekuja muda mchache baada ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Uyui, Tabora Dr. Kija Maige kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi watumishi wawili wa Afya wa Zahanati ya Ishihimulwa Rose Shirima na James Getogo waliohusika kwenye video ya mabishano iliyosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii

"Kwa mfano nimeona clip yaani Mtu anang’ang’ana kumpima Mgonjwa Malaria kwa kipimo ambacho kime-expire mwenzie anamwambia anatoa majibu ya hovyo, mwaka huu tutawajibishana" amesema Waziri Ummy