
Wamesema pamoja na lalamiko hilo kuwasilishwa kwa viongozi mbalimbali wa Wilaya kuonyesha ukubwa wa tatizo na madhara yanayoweza kutokea mfugaji huyo kuwa eneo la kilimo hakuna hatua iliyochukuliwa huku wakulima wa eneo hilo wakiendelea kuathiriwa na mifugo hiyo.
Akizungumza mbele ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Manyara RPC. George Katabazi, Ismail Sima (Mwananchi) alisema mfugaji aliyefahamika kwa jina la Lekombo anayeishi Kijiji cha Mbigiri Kata ya Partimbo amekuwa tishio kwani ameamua kuishi katikati ya eneo lililotengwa kwa shughuli za kilimo.
“Kijiji kilitenga eneo la kilimo, mifugo, makazi na hata hifadhi ili kuepuka mwingiliano wa shughuli za kibinadamu, hili mwenzetu aliamua kununua ardhi ekari kumi akidai kutaka kulima lakini baadaye aliamua kuhamia na mamia ya mifugo yake hapo ambayo kila kukicha wakulima hatuna amani..mifugo inaingiza shambani na kuharibu mazao” Alisema Sima.
Ibrahimu Musa, Kiongozi wa Dini (Bakwata) alisema pamoja na suala hilo kuwasilishwa kwa Wakuu wa Wilaya zaidi ya watatu Kiteto kwa nyakati tofauti ya kipindi chao hakuna aliyeweza kulitatua huku akisema madhara huwa yanatokea kwa wakulima mazao yao kuharibiwa na mifugo na hata kutishiwa amani akisema inaweza kutokea siku moja mkulima atachoka na hali hiyo na kuamua kuchukua sharia mkononi” alisema.
Akizungumzia migogoro hiyo Katibu wa mila wa jamii ya kifugaji maasai, Shukumu Tuke alisema migogoro ya ardhi Kiteto imepungua kwa kiasi kikubwa kufuatia kuwekwa misingi na mahusiano baina ya pande hizo kukutana mara kwa mara kuzungumzia changamoto hizo.
“Tunashukuru sana Serikali ya Kiteto imetuunganisha wafugaji na wakulima kila mara huwa tunakutana kuzungumzia changamoto na kuzitatua hivyo kwa niaba ya wafugaji, RPC Katabazi sisi tutakupa ushirikiano kwa kipindi chote utakapokuwa Manyara kutokomeza migogoro hii” alisemaTuke Katibu wa mila jamii ya wafugaji.
Hata hivyo RPC Katabazi katika kikao hicho aliomba makundi hayo ushirikiano na Jeshi la Polisi akisema haliwezi kufanikiwa kulinda raia na mali zao endapo litakosa ushirikiano, hivyo amewata viongozi hao kukutana na maafisa wa Polisi waliopo kwenye Kata ili kuendelea kushuhulikia changamoto hizo
Kuhusu mfugaji huyo aliyeamua kubadilisha matumizi ya eneo hilo na kuishi katikati ya eneo la kilimo RPC Katabazi amemwagiza OCD Kiteto kukutana na Mkuu wa Wilaya kushughulikia hilo na kama litashindikana washirikishe uongozi wa mkoa kwani hakuna aliye juu ya sharia na kama kuna mipango ilipangwa na Serikali ya kijiji kwa manufaa ya wananchi wote basi isimamiwe kiAkamilifu.