Waziri Jenista ameyasema hayo jijini Mwanza wakati akizungumza na watumishi katika ofisi ya mkuu wa mkoa huo ndipo akawataka kuzingatia maadili ya utendaji wao wa kazi na kutaka halamshauri ambazo watumishi wake hawazingatii maadili kuchunguzwa
‘Inavyoonekana bado zipo halmashauri hazizingatii maadili ya utumishi wa umma tumeshawaagiza tume ya utumishi wa umma nchini kuanza kuzifuatilia halmashauri hizo kwa karibu tunae mkaguzi mkuu wa serikali anayekagua mahesabu CAG lakini utendaji kazi waw a mwajiri na mtumishi mkaguzi wetu mkuu ni tume ya utumshi wa umma sasa tunatengenza mfumo utakaotusaidia kukagua utendaji kazi wa kila taasisi ya umma nchini’







