
Bado haijabainika iwapo kulikuwa na mabishano kati ya mlinzi huyo na Kanali Engola.
Askari huyo ambaye bado hajatambulika rasmi, alijiua kwa kujipiga risasi dakika chache baadaye.
Baadhi ya walioshuhudia walisema askari huyo alizunguka eneo jirani na sehemu hiyo akifyatua risasi hewani.
Kanali Engola alikuwa afisa mkuu wa serikali, na hapo awali aliwahi kuwa naibu waziri wa ulinzi.
Spika wa bunge la Uganda alithibitisha kifo cha Kanali Engola katika taarifa fupi alipokuwa akiongoza kikao cha asubuhi bungeni