Jumatatu , 24th Oct , 2022

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Rishi Sunak (42), amewaahidi Waingereza kuwa atawahudumia kwa uadilifu na unyenyekevu  na kusema licha ya Uingereza kuwa ni nchi kubwa lakini inakabiliwa na changamoto za kiuchumi na kusisitiza utulivu na umoja.

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Rishi Sunak (42)

Rishi Sunak, amethibitishwa kuwa kiongozi anayefuata wa chama cha Conservative, na Waziri Mkuu baada ya kuwa mgombea pekee baada ya mgombea mwenzake Penny Mordaunt kujiondoa kabla tu ya muda kuisha, ambapo katika hotuba yake amesisitiza.

Sunak amesema "Nanyenyekea na kuheshimu kuungwa mkono na wabunge wenzake na kuchaguliwa kuwa kiongozi, ni bahati kubwa maishani mwangu kuweza kutumikia chama ninachokipenda na kurudisha nchi ninayodaiwa sana."