Jumapili , 14th Mei , 2023

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa taarifa kuhusu tetesi za uwepo wa mlipuko mpya wa Covid 19 Tanzania ambapo amewataka Wananchi waondoe hofu na kusema Wizara ya Afya inachakata taarifa zilizokusanywa kutoka Hospitali/Vituo mbalimbali ndani ya wiki hii kisha watatoa taarifa.

Aidha Waziri Ummy amesema “Kwa taarifa za Wagonjwa waliopimwa virusi vya Covid-19 wiki ya kuanzia May 6 - 12, 2023, Watu 6 kati ya 288 walithibitishwa kuwa na corona ikiwa ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya April 29 hadi May 05,2023, hakuna kifo chochote kilichothibitishwa kusababishwa na Covid-19”

“Wizara ya Afya inaendelea kufuatilia kwa karibu kwenye Hospitali mbalimbali na tutawapa taarifa kamili, nawaomba Wananchi muendelee kuzingatia kanuni za afya na usafi”