
Lee Sang-min amekuwa akikabiliwa na shinikizo kubwa la kujiuzulu kufuatia kisa hicho kilichosababisha vifo vya watu 156 na wengine 152 kujeruhiwa ajali iliyotokea mwezi Oktoba 29 mwaka huu.
Bunge linalodhibitiwa na upinzani lilipitisha hoja hiyo siku ya leo. Lakini Rais Yoon Suk-yeol anatarajiwa kukataa wito wa kujiuzulu kwa waziri wake. Chama cha Democratic kimetishia kumshtaki waziri huyo iwapo rais atakataa hoja hiyo, shirika la habari la Yonhap limeripoti.
Polisi wa nchi hiyo wamekosolewa kwa namna ambavyo walilelta uzembe kwenye ajali hiyo , iliyotokea katika wilaya maarufu ya Seoul yenye baa na migahawa mingi.
Ajali hiyo ilitokea wakati wakati umati wa watu ulikusanyika kusherehekea Halloween bila vizuizi kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa Covid.