Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola ajiuzulu

Alhamisi , 23rd Jan , 2020

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekubali ombi la kujiuzulu kwenye nafasi yake ya Uwaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola kutokana na sababu mbalimbali.

Rais Magufuli

Rais Magufuli amesema hayo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa nyumba 12 za Askari Magereza kwenye Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam, ambapo ameeleza kulikuwa na mkataba ambao ni wa ajabu.

Rais Magufuli amesema kuwa "ninajua Waziri wa Mambo ya Ndani hayupo hapa ameshaandika barua ya kujiuzulu na mimi nimeshamkubalia"

"Palikuwa na mkataba wa ajabu unatengenezwa mambo ya ndani, wa zaidi ya Tril. 1 na umesainiwa na Kamishna wa Fire,na haujapangwa na kupitishwa na Bunge, wakati wa vikao na kampuni moja walipokuwa wakienda kwenye mkutano walilipana pesa nyingi" ameongeza Rais Magufuli