Jumanne , 10th Mei , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii nchini kuacha kuwekeza kwenye majengo ambayo hayanafaida kwa wananchi wa wakawaida na badala yake wawekeze kwenye viwanda.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Magufuli,

Akizungumza jana kwenye Uzinduzi wa Majengo ya PPF na NSSF jana Jijini Arusha, Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa endapo mifuko hiyo ingetumia fedha ambazo inajenga kwa thamani kubwa na kuwekeza kwenye viwanda ingewasadia wananchi wengi zaidi kuliko majengo wanayoyajenga kwa sasa.

Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa endapo Mifuho hiyo yaHhifadhi ingejikita hata kwenye uwekezaji wa viwanda vya sukari pamoja na uagizaji wa bidhaa hiyo Tanzania isingekuwa na tatizo hilo ambalo linalikabili taifa kwa sasa.

Dkt. Magufuli amesema kuwa kuna uwezekano wa bidhaa hiyo ambayo imekua adimu nchini kwa Sasa kubatikana kwa bei rahisi na kwa wingi zaidi endapo mifuko hiyo ingejikita katika uwekezaji katika sekta hiyo.

Rais Dkt. Magufuli ameitaka mifuko hiyo ibadilike kimtazamo katika maendeleo ya Taifa hasa kwa serikali yake ya awamu ya tano ili kuendana na kasi ya maendeleo ambayo yatagemea kukua kupitia kwa uchumi wa viwanda.

Aidha, Rais amesema mifuko kama hiyo katika nchi za nyingine dunia inaliingiza patoa kubwa taifa tofati na nchini Tanzania na kusema kuwa kuna maeneo ya kurekebisha ili mifuko hiyo iongeze pato la taifa na kukuza uchumi wa nchi.

Sautri ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Magufuli, akiongelea pato la taifa kupitia hifadhi za Jamii
Sauti Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Magufuli, akiongelea uwekezaji katika viwanda