
Vifaa tiba vilivyotolewa ni pamoja na dawa, mashuka na vifaa vya usafi vimetolewa na Chuo Cha Usimamizi wa Fedha IFM Kampasi ya Mwanza ili kutimiza azma ya serikali ya kupunguza vifo vya mama wajawazito na Watoto wachanga ambapo katika Zahanati hiyo ya Kirumba kinamama hamsini hadi sitini hujifungua kila mwezi
Kwa upande wake Dkt Eusebi John ambae ni Kaimu Meneja wa Chuo Cha IFM Mwanza amesema chuo hicho kimekuwa kikifanya shughuli mbalimbali za kijami.