Jumamosi , 18th Mei , 2019

Kufuatia mapema mwaka huu aliyekuwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif kujiunga na ATC Wazalendo, chama hicho cha siasa kimeendelea kujikusanyia wanachama wapya wakiunga kauli ya Shusha Tanga Pandisha Tanga.

Wanachama Wapya waliojiunga na ACT Wazalendo leo.

Zaidi ya wanachama wapya 1000 wamejiunga na chama hicho leo, ambapo zaidi ya 500 ni kutoka mkoa wa Kaskazini Pemba na wengine zaidi ya 600 kutoka Jimbo la Mtambile, Wilaya ya Mkoani katika Mkoa wa Pemba Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya uongozi ya Mkoa Kaskazini Pemba, leo Mei 18, 2019 ilikuwa katika hatua ya kuiendeleza operasheni ya  Shusha Tanga Pandisha Tanga na kufanikiwa kuvuna wanachama hao wapya.

''Asubuhi ya leo Kamati ya uongozi ya Mkoa Kaskazini Pemba ilikuwa katika Jimbo Gando kwa lengo la kuwapa kadi wanachama wapya katika matawi yaliyomo ndani ya jimbo na jumla ya Wanachama Wapya 500 wamekabidhiwa kadi'', imeeleza taarifa hiyo.

Aidha taarifa imeendelea kueleza kuwa, jumla ya Wanachama 652 wamechukua Kadi kwa malipo Jimbo la Mtambile  huku wakiejinadi kuwa, katu kurudi nyuma sio rahisi Chama Makini kama ACT Wazalendo kinaendelea Kupandisha Tanga.