Alhamisi , 23rd Apr , 2015

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)imesema kuwa emeandikisha watu zaidi 300,000 na kuwa imekamilisha katika mkoa huo na itaanza mwezi mei katika mikoa ya Dodoma, Mbeya, Rukwa na Katavi na mwezi huu ikianza katika mikoa ya Iringa, Ruvuma,Lindi na Mtwara

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Damian Lubuva akifafanua jambo.

Akizungumza kwa njia simu mwenyekiti wa tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Damian Lubuva amesema kuwa zoezi BVR kwa mkoa wa Njombe limekamilika na kuwaandikisha wananchi zaidi ya 380,000 katika mkoa huo.

Jaji Lububa amesema kuwa baada ya kukamilika mkoani Njombe zoezi hilo linaelekea katika mikoa ya Iringa, Ruvuma, Lindi na Mtwara ambapo linatarajiwa kuanza Aprili 24, mwaka huu.

Amesema kuwa mbali ya mikoa hiyo ambayo imeanza mwezi huu pia ilitaanza ndani ya mwezi Mei ambayo ni pamoja na mikoa ya Dodoma, Mbeya, Rukwa na Katavi.

Amesema kuwa katika mkoa wa Njombe limefanikiwa vizuri kwa kuandikisha watu zaidi ya 380,000, na kuwa haoni sababu ya uchaguzi mkuu kuahirishwa Oktoba, kwa sababu wana vifaa 1,600 kwa sasa kutoka 250 vilivyokuwepo awali, na kwamba wiki ijayo wanatarajia kupata 1,600, na hivyo kufikia 3,200 ambavyo watavitumia katika mikoa ya Iringa, Ruvuma, Lindi na Mtwara inayotarajia kuanza zoezi la uandikishaji.

Lubuva amesema wanatarajia hadi kufikia mwezi Mei vifaa vyote vitakuwa vimekuja na hivyo kufikia idadi ya mashine 8,000 ambazo zitafanya zoezi hilo kufanyika katika mikoa yote iliyobaki nchini.

“Mkoa wa Njombe zoezi limeenda vizuri na tumefanikiwa kuandikisha watu laki tatu na themanini hivyo sioni sababu ya uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu kuahirishwa,” alisema Lubuva.

Aidha Lubuva aliongeza kuwa pamoja na changamoto zilizojitokeza katika mkoa wa Njombe, Lubuva alisema zoezi hilo lililomalizika Jumamosi iliyopita lakini limefanyika kwa mafanikio.

Kuhusu zoezi hilo kurudiwa katika kata za Mjimwema amesema hakuna mwananchi aliyejitokeza akaachwa na yeye kama Mwenyekiti anasema hakuna yeyote aliyejitokeza.

Aidha amesema kuwa hakuna sababu ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kuahirishwa Oktoba mwaka huu, kwa kuwa zoezi la uandikishaji wananchi kupitia mfumo mpya wa kielektroniki (BVR) litakuwa limemalizika.

Kauli hiyo ameitoa wakati atoa tathmini ya zoezi la uandikishaji katika mkoa wa Njombe na mwelekeo wa tume hiyo kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba.