
Nembo ya Tigo (kushoto) na Zantel (kulia)
Taarifa hiyo imetolewa leo Novemba 4, 2019, na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Simon Karikari, ambapo amesema kuwa hatua ya muunganiko wa makampuni haya mawili, imekuja baada ya taratibu zote za kisheria na kiumiliki kukamilika na kwamba lengo kuu ni kukuza na kuboresha huduma za mawasiliano nchini.
"Ninaamini kuwa kuunganishwa kwa kampuni hizi, Tigo na Zantel kutajenga huduma jumuishi kwa watanzania wote siku za usoni, wateja wote wa Tigo na Zantel, wataweza kufurahia huduma bora kutoka kwenye soko imara litakalosaidia kuchochea ubunifu kwenye sekta ya mawasiliano" amesema Karikari.
Muunganiko huu utawezesha kupanua wigo wa huduma pamoja na kuongeza ubora wa upatikanaji wa mawasiliano katika maeneo ya mijini na vijijini.