Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe aliyevaa Kofia (Kibaraghashia) akiwa na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe.
Hussein Bashe amekanusha na kufafanu kwamba kumefanyika mabadiliko makubwa sana katika Muswada na kwamba wabunge wa CCM wamefanya wamebadiliko makubwa.
Bashe ameeleza kwamba mabadiliko hayo waliyoyafanya wameongozwa na Katiba, "haki za Raia Ibara ya 18, 20 na pia ibara ya 38,39 na 42 zimetuongoza sana ili kuto create vacuum ya uongozi".
Hata hivyo baada ya utetezi huo, Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amemuambia Mbunge huyo kuwa hataweza kuamini, mpaka aone ratiba ya mabadiliko.
"Hatuamini mpaka tuone schedule of amendments maana Katibu Mkuu wenu alishasema kuwa msibadili hata koma. Ina maana mmeenda kinyume na Katibu Mkuu, Mwalimu Bashiru Ali", amesema Zitto Kabwe.


